Sunday, July 15, 2012

TUNZA NGOZI YAKO


Ili ngozi iweze kuwa na mvuto inahitaji matunzo, ngozi inayoachwa bila matunzo kamwe haiwezi kuwa na mvuto,ngozi inaweza kutengenezwa kupitia vipodozi vinavyotengenezwa na kemikali mbalilmbali,lakini pia inaweza kutunzwa kupitia viasilia mbalimbali vitokanavyo na mimea au mazao ya shambani.
Matunda ya aina mbalimbali yanasaidia sana katika kutunza ngozi yako.matunda kama Tango na maparachichi hutumika katika kutunza ngozi kwa kula pamoja na kupaka usoni.
Kwani pendelea kula aina hii ya matunda na pale unapopata muda chukua tango lako lipondeponde changanya na mayai na alovera kisha zisage vizuri baada ya hapo paka usoni, shingoni au popote mwilini subiri dakika 20.
Baada ya hapo safisha uso wako unaweza kufanya hivi mara kwa mara kila wiki.ili kutunza ngozi yako na ikishindikana waone wataalamu wa masuala ya ngozi kiutaalamu zaidi.
KUTUNZA NGOZI YAKO.

  1.  Epuka uvutaji wa aina yoyote, mfano sigara bangi  madawa ya kulenya, petrol, na mambo mengine kama hayo. Kuvuta kuna madhara mengi kiafya kwenye mwili pamoja na magonjwa ya moyo na cancer ya mapafu.Hata hivyo kitu watu wengi hawajui ni kwamba nicotine ambayo iko kwenye sigara unapovuta inaweza kubadilisha rangi ya ngozi na wakati mwingine kuota chunusi.Ili uweze kuwa na ngozi nzuri ni lazima uache kabisa kuvuta.
  2. Vitamin A na E , wakati unaendelea kuwa mtu mzima ngozi inaanza kupoteza uzuri wake, kwa sababu cell, collagen na elastin zinaanza kupungua nguvu matokeo yake ni wrinkles na matatizo mengine ya ngozi. Matumizi ya vitamin A na E supplement zenye ( collagen na elastin) vyaweza kuzuia ngozi kuharibika. Vitamin A na E pamoja na madini ya asili vimethibitisha kuongeza uwezo wa cell za ngozi, hivyo inaongeza ubora na muonekano wa ngozi.
  3. Epuka kutumia mafuta ya mgando kwenye ngozi, mafuta yanaziba pols na kusababisha chunusi, chunusi zaweza kusababisha makovu usoni , na hivyo kupoteza kabisa muonekano mzuri wa ngozi yako. Wakati unapotumia product za ngozi tumia mabazo hazina mafuta pia ambazo  hazina harufu ( fragarance).

    Punguza matumizi ya sukari, haswa soda na chai, matumizi ya vyakula vya kukaanga, kama chips na vinginevyo. Nyama nyekundu na maziwa ( diary product) unashauriwa kuacha kabisa kwa sababu mara nyingi husababisha allergy. Kunywa maji mengi, kula matunda na mboga za kutosha, lala mapema ikiwezekana kabla ya saa tatu na nusu. Usioshe uso na sabuni.

Jinsi ya kufanya mask

Mask
siku zote huleta faida kubwa sana kwa ngozi zetu, hata hivyo, ni muhimu kujua jinsi vizuri kuomba tu wakati unaweza kufanya matumizi kamili ya mali zao na kufikia matokeo ya kushangaza Kuna tofauti masks ambayo yanaweza kufanyika ... katika saluni , kununuliwa katika duka au kujiandaa kujitegemea Hii mkono-alifanya hasa kukubaliwa na wanawake kwa sababu ni ya asili na gharama nafuu. Hapa ni vidokezo juu ya jinsi ya kufanya
mask. Kujua aina ya ngozi una na nini mahitaji yao.. Kuna tofauti nyingi masks au vipengele ambavyo ni mmoja mmoja kulengwa kwa aina fulani ya ngozi na mahitaji yake. Kuna sheria nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa masks nyumbani, una kuchagua moja kuwa ni bora kwa ajili yenu na kuwapa ngozi yako kila kitu ni mahitaji Kama wewe ni mtetezi wa masks pet, chagua.tayari-alifanya masks katika
drugstore. kabla ya kuomba mask, wewe kabisa lazima kusafisha ngozi yako mask Hii itakuwa bora kufyonzwa ndani ya ngozi.. Yasafishe ili kufanya-up, kuifuta uso wako tonic, na kisha kuomba mask.
Omba mask kwa mujibu wa maelekezo ya chupa, yaani, uso mzima, macho na kuepuka kinywa ngozi karibu na macho ni zaidi nyeti kuliko ya mapumziko ya ngozi
wakati mask. kazi maajabu juu ya ngozi yako, na kujaribu kupumzika.. Kama iwezekanavyo, kurejea kwenye baadhi ya muziki kufurahi yenyewe na kumngojea kwa utulivu na madhara ya mask
uangalifu kuondoa mask na safisha kulingana na maelekezo. Osha uso wako kwa maji vuguvugu na kuipangusa kwa kitambaa safi
. daima baada ya kuondoa mask, kuomba moisturizer juu ya uso wako.. Hii ni mara ya bora ya kutunza ngozi yako inaweza kuvuna faida zaidi kutokana na viungo ya creams moisturizing.

     
 faida za kunywa juisi katika mwili wa binadamu.
Kuna  juisi za aina mbalimbali na matumizi yake yanategemea na malengo ya mtumiaji. Inawezekana watumiaji wengi wanakunywa juisi bila kujua umuhimu au kazi yake mwilini.
Safu hii itaeleza utumie juisi gani  na wakati gani na nitaeleza pia jinsi ya kutengeneza na kazi zake.
JUISI YA TIKITI MAJI
Chukua tikiti maji (Watermelon), osha kisha likate vipande na chukua nyama yake ya ndani ambayo utaisaga na kupata juisi.
Faida yake
Juisi hii ina uwezo wa kusafisha figo pamoja na njia ya mkojo yaani Urethra. Inazuia unene (Obesity) kwa kuwa na kiwango kidogo cha calories.
JUISI YA KAROTI NA APPLE
Hutengenezwa kwa kusaga matunda hayo na kukamua maji yake na maelekezo yake yapo hapo chini.

JINSI YA KUTENGENEZA

Chukua kiasi cha karoti na apple kinachotosha kutengeneza juisi kwa kiasi ulichokusudia. Anza kuandaa juisi yako kwa kuosha na kumenya karoti na apple kisha katakata katika vipande vidogo vinavyoweza kusagika kirahisi kwenye blenda. Saga mchanganyiko wako ili upate juisi. Baada ya kupata mchanganyiko wa juisi yako unaweza kuongeza asali japokuwa siyo lazima kwa kuwa matunda hayo yana sukari.

Faida yake

Juisi hii ina uwezo wa kutunza ngozi yako kwani tunda la apple linaondoa uchafu kwenye ngozi na karoti nayo kwa kutumia kirutubisho cha beta-karotini chenye uwezo wa kutengeneza vitamini A huweza kulinda na kurejesha uhai katika ngozi ambapo inaifanya ionekane nyororo.
 Pia juisi hii huweza kulifanya tumbo lako kuwa safi kwani husafisha tumbo na kuondoa uchafu tumboni. Aidha, juisi hii inafanya ini lifanye kazi yake vizuri kwa kulainisha nyongo na kusaidia kuondoa uchafu.

JUISI YA VIAZI MVIRINGO

Chukua viazi mviringo vinavyotosha kwa juisi. Andaa kwa kuviosha na kumenya kisha katakata vipande vidogo kwa ajili ya kuvisaga. Saga ili upate juisi uliyoikusudia.
Faida yake
Juisi hii inatumika kama dawa ya kuondoa au kupunguza asidi au gesi tumboni. Juisi ya viazi mviringo inaweza kusaidia kupunguza matatizo ya figo, kisukari, unene au kitambi.

JUISI YA MBOGAMBOGA

 Juisi hii ina mchanganyiko wa mbogamboga ambazo mtumiaji hupenda kama vile matango, karoti na nyanya. Maandalizi yake ni kama juisi nyingine.
Anza kwa kuosha mbogamboga hizo kisha menya na kukatakata vipande. Saga mchanganyiko huo kwenye blenda ili upate juisi uliyoikusudia.

Faida yake

Juisi hii inasaidia kuzuia kansa hasa ile ya kwenye mfumo wa kumeng`enya chakula, kukinga mapafu na mishipa ya artery. Pia inasaidia kuimarisha kinga.
Kwa aina hizo chache za juisi unaweza kujua umuhimu wa juisi za matunda na mbogamboga tunazotumia. Kwa leo ninaishia hapo, siku zijazo nitaendelea kukupatia ufahamu kwa aina zingine za juisi pamoja na kazi zake.

No comments: