MAJINA YA HAWA HAKUNA NDUGU YAKO??
-WALALA HOI WALALAMIKA, WALITOA SH30,000 ZA MAOMBI ‘ZIMEENDA NA MAJI’
Patricia Kimelemeta- MWANANCHI
- majina yanayosomeka ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama;
Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia,
Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Pereira Ame Silima.
-Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi
na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni
Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
-Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa
Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa
Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es
Salaam, Suleinan Kova.
Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na
Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), Ludovick Utouh na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.
Kwa upande wa wabunge wamo Dk
Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo
Filikunjombe; Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa
Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril
Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.
Wengine
ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa
Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.
Wabunge
wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu
CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.
Orodha
hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya
viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba,
Suzan Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary
Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.
Mkurugenzi apatwa kigugumizi
Mkurugenzi
wa Manispaa hiyo, Magreth Nyalile alipoulizwa kuhusu orodha hiyo
alisema kuwa, majina hayo hajayaona na kwamba waliobandika wamefanya
uamuzi huo bila ya yeye kuupitia.
“Majina yenyewe sijayaona,
hivyo basi siwezi kujua ni kina nani waliopewa viwanja hivyo, kwa sababu
wako zaidi ya 1,000, jambo ambalo litakuwa vigumu kwangu kubaini tatizo
hilo,” alisema Nyalile.
No comments:
Post a Comment