UTHIBITI WA SARATANI AU KANSA...
Upasuaji
Kinadharia, aina za saratani // kansa zisizo za kihematolojia zinaweza kutibiwa kama zitaondolewa kabisa kwa upasuaji, lakini jambo hili huwa haliwezekani kila wakati. Wakati kansa // saratani imeenea kwenye maeneo mengine ya mwili kabla ya upasuaji, utoaji kamili kwa kufanyia upasuaji kwa kawaida hauwezekani. Katika muundo wa Halstedia wa jinsi kansa // saratani inavyoendelea, uvimbe hukua ndani (ya seli moja), kisha kuenea kwenye limfu nodi, kisha kwenye sehemu zingine za mwili. Jmabo hili limesababisha umaarufu wa tiba za ndani pekee (sehemu iliyoathiriwa) kama vile upasuaji wa saratani ndogo. Hata uvimbe mdogo ulio katika sehemu moja unaendelea kutambulika kama ulio na uwezo wa kuenea.Mifano ya taratibu za upasuaji wa kansa // saratani ni pamoja na mastektomia(upasuaji wa matiti) kwa kansa // saratani ya matiti, prostatektomia (upasuaji wa tezi kibofu) kwa kansa // saratani ya tezi kibofu, na upasuaji wa kansa // saratani ya mapafu kwa kansa // saratani ya seli zisizo ndogo za mapafu. Lengo la upasuaji linaweza kuwa ama kuondolewa kwa uvimbe pekee, au sehemu nzima ya mwili // ogani. Seli moja ya kansa // saratani haiwezi kuonekana kwa macho lakini unaweza kukua tena na kuwa uvimbe mpya, mchakato uitwao kutokea tena. Kwa sababu hii, mwanapatholojia atachunguza Sampuli iliyotolewa ili kuamua ikiwa ina kiasi kidogo cha tishu zilizo na afya // zisizo na ugonjwa, na hivyo kupunguza uwezekano wa kuwa seli ndogo kabisa za kansa // saratani zimesalia katika mgonjwa.
Juu ya kuondolewa kwa uvimbe msingi, upasuaji mara kwa mara ni muhimu kwa kuamua hatua ulipofika ugonjwa, kwa mfano, kuamua kiwango cha ugonjwa huo na kama umeenea hadi limfu nodi za eneo hilo. Uamuzi wa hatua ulipofika ugonjwa ni kiukilia kikubwa cha utambuzi wa ugonjwa na haja ya tiba itakayosaidia.
Mara kwa mara, upasuaji ni muhimu kudhibiti dalili, kama vile kubanwa kwa uti wa mgongo au kuzibwa kwa uchengelele. Jambo hili linajulikana kama matibabu ya kutuliza // kupunguza.
Matibabu kwa njia ya eksirei
Matibabu kwa njia ya eksirei yanaweza kutumika kutibu karibu kila aina ya uvimbe imara, ikiwa ni pamoja na saratani // kansa ya ubongo, matiti, mlango wa uzazi, zoloto, mapafu, kongosho, tezi kibofu, ngozi, tumbo, uterasi, au sarkomasi yenye tishu laini. Mnururisho pia hutumiwa kutibu lukemia na limfoma. Kipimo cha mnururisho kwa kila eneo hutegemea mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kiwango cha hisi kwa mnururisho cha kila aina ya kansa // saratani na kama kuna tishu na viungo vilivyo karibu vinavyoweza kuharibiwa na mnururisho. Kwa hiyo, kama ilivyo na kila aina ya matibabu, matibabu kwa njia ya eksirei yana madhara yake.
Tibakemo
Kwa sababu baadhi ya madawa hufanya kazi vyema zaidi yakiwa pamoja kuliko yakiwa peke yake, aina mbilia au zaidi za madawa mara nyingi hupeanwa kwa wakati mmoja. Jambo hili linaitwa "tibakemo iliyochanganywa"; madawa mengi ya tibakemo hupeanwa kwa kuchanganywa.[5]
Matibabu ya baadhi ya lukemia na limfoma yanahitaji matumizi ya dozi ya juu ya tibakemo, na mnururisho wa mwili wote (TBI). Matibabu haya huyeyusha uboho, na hivyo uwezo wa mwili kupona na kujaza damu tena. Kwa sababu hiyo, uboho, au kuvuna seli za shina la damu zilizo pembeni hufanywa kabla ya sehemu ya matibabu inayohusisha uyeyushaji, ili kuwawezesha "kuwaokoa" baada ya matibabu imepewa. Jambo hili linajulikana kama uatikaji wa seli za shina kutoka mwili mmoja. Vinginevyo, seli za shina zinazohusishwa na damu zinaweza kuatikwa kutoka kwa mfadhili asiyehusika lakini aliye na seli zinazofanana.(MUD).
Matibabu ya kulenga
Matibabu ya kingamwili ya aina moja ni mkakati mwingine ambapo wakala wa matibabu ni kingamwili ambayo hasa hujifunga kwa protini kwenye uso wa seli za kansa // saratani. Mifano ni pamoja na anti-HER2/neu kingamwili ya trastuzumab (Heseptini) inayotumika katika kansa // saratani ya matiti, na anti-CD20 kingamwili rituksimabu, inayotumika katika aina mbalimbali za madhara // magonjwa ya Seli-B.
Matibabu ya kulenga pia yanaweza kuhusisha peptidi ndogo kama "vifaa elekezi" ambavyo vinaweza kujifunga kwa uso wa vipokezi vya seli au matriki iliyo nje ya seli iliyoathirika inayozunguka uvimbe. Radionuklidi zilizoambatishwa kwa peptidi hizi (mfano RGDs) hatimaye huua seli ya kansa // saratani ikiwa nuklidi itaharibikia katika sehemu zilizo karibu na seli hiyo. Hasa oligo au multima za motifu hizi zinazojifunga zina mvutio mkuu, kwa kuwa zinaweza kusababisha umaarum na shauku bora zaidi za uvimbe.
Matibabu kwa nguvu za mwangaza (PDT) ni matibabu ya kansa yenye awamu tatu na yanayohusisha kihisishamwanga, oksijeni ya tishu, na mwangaza (mara nyingi kwa kutumia leza). PDT inaweza kutumika kama tiba kwa kasinoma ya uso wa seli (BCC) au saratani ya mapafu, PDT pia inaweza kuwa muhimu katika kuondoa athari za tishu zenye madhara baada ya kuondolewa kwa uvimbe mkubwa kupitia upasuaji.[6]
Matibabu kupitia kingamaradhi
Uatikaji wa seli za shina za alojeni hematopoetiki ("uatikaji wa uboho" kutoka kwa mfadhili asiye na jeni zinazofanana) unaweza kuchukuliwa kama aina ya matibabu kwa kutumia kingamaradhi, kwani seli za kinga za mfadhili mara nyingi zitashambulia uvimbe huo katika tukio lijulikanalo kama athari za kipandikizi dhidi ya uvimbe. Kwa sababu hii, HSCT ya alojeni husababisha kuongezeka kwa kiwango cha kutibu kuliko uatikaji wa autolojia katika aina kadhaa za kansa, ingawa madhara pia ni makali zaidi.
Matibabu kwa kingamaradhi yanayohusu seli ambapo seli Asili za Kuua za wagonjwa (NK) na T-Limfositi za sitotoksi (CTL) hutumiwa yamekuwa yakitumiwa katika Ujapani tangu mwaka wa 1990. Seli za NK na CTL kimsingi huua seli za kansa wakati zimekuwa. Matibabu haya hupeanwa pamoja na aina zingine za matibabu kama vile upasuaji, matibabu kwa njia ya eksirei au tibakemo na hujulikana kama Matibabu ya Kuimarisha Kinga ya Aina Moja (Autologous Immune Enhancement Therapy) (AIET)[7][8]
Tiba kwa kutumia homoni
Vizuizi vya anjiojenesisi
Udhibiti wa dalili
Ingawa udhibiti wa dalili za saratani kwa kawaida haufikiriwi kama matibabu ya moja kwa moja ya kansa, ni kiukilia muhimu cha ubora wa maisha ya wagonjwa wa kansa, na una jukumu muhimu katika uamuzi wa iwapo mgonjwa anaweza kupokea matibabu mengine. Ingawa madaktari kwa ujumla wana ujuzi wa kimatibabu wa kupunguza maumivu, kichefuchefu, kutapika, kuhara, kutokwa na damu na matatizo mengine ya kawaida kwa wagonjwa wa saratani, taaluma mbalimbali na maalum za huduma za kupunguza zimeongezeka hasa katika kukabiliana na mahitaji ya udhibiti wa dalili ya kikundi hiki cha wagonjwa. Jambo hili hasa ni sehemu muhimu ya huduma kwa wagonjwa ambao magonjwa yao hayawezi kutibiwa kwa aina zingine za matibabu. Kwa kuwa matibabu mengi ya saratani huhusisha madhara ambayo kwa kiasi kikubwa hayapendezi // yana kera, mgonjwa aliye na matumaini madogo ya kupata tiba anaweza kuamua kutafuta huduma za kupunguza pekee, na kukwepa matumizi ya matibabu makali zaidi yanayompatia kipindi kirefu cha maisha ya kawaida.Madawa ya maumivu, kama vile afyuni na oksikodoni, na an, madawa ya kuzuia kichefuchefu na kutapika, hutumika sana katika wagonjwa walio na dalili zinazohusiana na saratani. Madawa bora ya kuzuia kutapika kama vile ondansetroni na analogu, pamoja na aprepitanti yamefanya matibabu ya haraka kuweza kufikiwa zaidi katika wagonjwa wa saratani.
Maumivu sugu kutokana na kansa karibu mara zote huhusishwa na tishu kuendelea kuharibika kutokana na utaratibu wa maradhi au matibabu (yaani upasuaji, matibabu kwa njia ya eksirei, tibakemo). Ingawa daima kuna jukumu la sababu za kimazingira na vurugu zinazoathiri katika mwanzo wa tabia za maumivu, hizi huwa si kwa kawaida sababu kuu za mwanzo wa magonjwa katika wagonjwa walio na maumivu ya saratani. Aidha, wagonjwa wengi walio na maumivu makali yanayohusiana na kansa wanakaribia mwisho wa maisha yao na huduma za kupunguzu dalili hizi zinahitajika. Masuala kama vile shutumu ya kijamii ya kutumia opioidi, hali za kazi na utendaji kazi, na matumizi ya huduma ya afya yanaweza kutokuwa muhimu katika udhibiti wa jumla wa kesi hiyo. Kwa hiyo, mkakati wa kawaida wa kudhibiti maumivu ya kansa ni kweka mgonjwa katika hali ya starehe iwezekanavyo kwa kutumia opioidi na madawa mengine, upasuaji, na hatua zingine za kawaida. Madaktari wamekuwa wakisita kuagiza dawa za kutia usingizi kwa maumivu katika wagonjwa wa kansa isiyotibika, kwa hofu ya kuchangia katika ulevi au kupunguza uwezo wa kupumua. Kikundi cha huduma za kupunguza, kikundi cha hivi karibuni kilichotoka kwenye kile cha hospice, kimesababisha uungaji mkono uliotanda zaidi wa matibabu ya kwanza zaidi ya maumivu kwa wagonjwa wa saratani preemptive.
Uchovu ni tatizo kubwa sana na la kawaida kwa wagonjwa wa kansa, na hivi karibuni tu ndipo limekuwa muhimu vya kutosha kuwafanya wanaonkolojia kupendekeza matibabu, hata kama lina nafasi kubwa katika hali ya maisha ya wagonjwa wengi.
Utafiti
Majaribio ya kikliniki ni mojawapo ya hatua za mwisho za mchakato wa muda mrefu na wa makini wa utafiti wa kansa. Utafutaji wa matibabu mapya huanza katika maabara, ambapo wanasayansi kwanza hubuni na kuchunguza mawazo mapya. Kama njia inaonekana kuwa na matumaini, hatua inayofuata inaweza kuwa upimaji wa matibabu katika wanyama ili kuona jinsi inavyoathiri kansa katika viumbe hai na kama ina athari zinazodhuru. Bila shaka, matibabu yanayofanya kazi vyema katika maabara au katika wanyama si lazima yafanyekazi vizuri katika watu. Tafiti hufanywa kwa kutumia wagonjwa wa saratani ili kutambua ikiwa matibabu yanayoonyesha uwezo wa kufanya kazi ni salama na bora.
Wagonjwa wanaoshiriki wanaweza kusaidiwa na matibabu wanayoyapokea. Wao hupata huduma za kisasa kutoka kwa wataalamu wa kansa, na wao hupokea ama matibabu mapya yanayofanyiwa majaribio au matibabu bora zaidi ya kawaida yanayopatikana ya kansa wanayougua. Wakati uo huo, matibabu mapya pia yanaweza kuwa na hatari zisizojulikani, lakini kama matibabu mpya yanaonekana kufanya kazi vyema au zaidi zaidi ya matibabu ya kawaida, wagonjwa wa utafiti wanayoyapokea wanaweza kuwa kati ya watu wa kwanza kunufaika. Hakuna thibitisho kwamba matibabu mapya yanayofanyiwa majaribio au matibabu ya kawaida yataleta matokeo mazuri. Katika watoto walio na kansa, utafiti wa majaribio ulipata kwamba wale waliojiunga na majaribio hawakuwa kwa wastani na nafasi ya kuwa katika hali bora au mbaya zaidi ya afya wakilinganishwa na wale waliokuwa wakipokea matibabu ya kawaida; jambo hili linathibitisha kwamba kufanikiwa au kutofanikiwa kwa matibabu ya majaribio hakuwezi kutabirika.[10]
Matibabu ya kukamilishana na ya mbadala
Katika mimba
Matukio ya kansa kuwepo kwa wakati mmoja na mimba yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa umri wa mama wajawazito[15] , na kutokana na ugunduzi wa kuwepo kwa uvimbe katika mama wajawazito wakati wa majaribio yanayofanywa kabla ya mtoto kuzaliwa.Matibabu ya kansa yanahitaji kuchaguliwa ili kupunguza madhara kwa mama na mtoto wake. Katika baadhi ya matukio kutolewa kwa mimba kwa sababu za kimatibabu kunaweza kupendekezwa.
Matibabu kwa njia ya eksirei kwa jumla hayawezi kutumika, na daima tibakemo huwa na hatari ya kusababisha kuharibika kwa mimba na ulemavu wa kuzaliwa nao.[15] Ni mambo machache sana yanayojulikana kuhusu madhara yanayosababishwa na madawa kwa mtoto.
Hata kama dawa fulani imechunguzwa na kuonekana kuwa haipiti kondo na kumfikia mtoto, aina zingine za saratani zinaweza kudhuru kondo na kuifanya dawa kupita // kupenyeza.[15] Aina fulani za saratani ya ngozi zinaweza hata enea hadi kwa mwili wa mtoto.[15]
Utambuzi pia hufanywa kuwa mgumu zaidi, kwani tomografia kwa kutumia compyuta haiwezekani kwa sababu ya kipimo chake cha mnururisho kilicho juu. Hata hivyo, upigaji picha kwa kutumia mwangwi wa sumaku hufanya kazi kama kawaida.[15] Hata hivyo, vyombo vinavyohitilafiana haviwezi kutumiwa, kwani huwa vinavuka kondo.[15]
Kutokana na matatizo ya kufanya utambuzi mzuri na matibabu saratani wakati wa ujauzito, njia mbadala ni ama kufanyiwa upasuaji wakati mtoto ametimiza kiwango cha kujitegemea ili kuanza matibabu ya kina zaidi ya kansa, au, kama kansa ni mbaya kiasi kwamba mama hawezi kusubiri kwa muda huo wote, basi mimba hutolewa ili kuitibu kansa hiyo.[15]
No comments:
Post a Comment