Friday, October 18, 2013

MATUMIZI SAHIHI YA CONDOM

Wanaume wengi hawajui matumizi sahihi

Kondomu  zimetengenezwa kwa sura na maumbile, rangi mbalimbali tofauti  ambazo baadhi yake kwa hakika zinavutia kuzitazama.

Hadi sasa, zipo zenye harufu au marashi anuwai kama yale ya ndizi, zabibu, chokoleti na hata zile zenye harufu ya Big G.
 Tukizungumzia kinga bora ya magonjwa ya ngono na mimba sizizotarajiwa hii bidhaa inashika namba moja.

Condom haidhuru mtu yeyote kama zilivyo kinga nyingine za kuzuia mimba ambazo huwasababishia mateso makubwa sana wanawake na wakati mwingine kuwabadilisha kabisa kiakili na kimwili.

Sikatai kila kitu kina side effects zake, lakini jamani nani amewahi kuugua kwa sababu tu katumia Condom?
 Kutumia kondom ya wanaume
 
Condom kwa Tayo
Jinsi ya kutumia kondom TAYO
  • Hakikisha umeangalia mda wa matumizi wa kondom uliyonayo. Kama mda wake (expiry date) wa matumizi umekwisha basi haikufai. Fungua kipakiti chenye kondomu wakati tu ukiwa tayari kuitumia. Bila hivyo yale mafuta mafuta maalum kwenye kondomu yatakauka.
  • Unapofungua pakiti kuwa mwangalifu usiipasue, au kuitoboa wala kuiharibu kondom yenyewe. Ikipasuka itupilie mbali na uchukue nyingine.
  • Kondomu huwa zimesokotwa na kuwa kama duara. Kuivaa, ile sehemu ya mafuta mafuta inapaswa kuwa nje.
  • Hivyo basi ivae kwa kuikunjua kuanzia kwenye ncha (kichwa)cha uume.
  • Ishike sehemu ya chuchu ya kondomu kwa kutumia dole gumba na kidole chako cha kwanza ili kutoa hewa kutoka sehemu hiyo, ili manii yahifadhiwe mahali hapo pale yatakapotoka.
  • Sasa Endelea kuishikilia kondom kwa mkono mmoja. Kwa kutumia mkono wa pili ikunjue hadi kufikia kwenye mavuzi yaani kwenye shina la uume. Kama mtumiaji hajatahiriwa anapaswa kuvuta lile govi la uume wake kabla ya kuvaa kondomu. Kama kondomu haina kilainishi cha kutosha, vilainishi au majimaji (kama vile silicone, glycerine, au K-Y jelly) vyaweza kuongezwa kwa nje. Tahadhari mafuta kama yale ya kupikia, ya kujipaka mwilini kama kama vile Vaseline hayafai kutumiwa kama kilainishi.
  • Baada ya kufanya mapenzi kondomu inapaswa kuvuliwa kwa njia sahihi pia. Baada tu ya kufika kilele na kutoa manii, mwanaume anapaswa kuutoa uume wake kutoka ukeni, kabla haujalegea kabisa, kwani akichelewa huenda kondom ikatumbukia ukeni mwa mwanamke. Kisha ashikilie kondomu kutoka shinani mwa uume na kuivua taratibu pasi na manii kumwagika.
  • Unaweza kuifunga kondom kwenye karatasi na kuitupa kwenye choo cha shimo
  • Usitupe kondom kwenye hooni cha kupiga maji kwani huenda ikatatiza utendaji kazi wa choo hicho.
  • Tumia kondom nyengine kwa kila tendo jengine la kujamiana. Tumia kondom kila wakati unapofanya mapenzi.

No comments: