Monday, July 16, 2012

CHUNUSI NA USONI

Chunusi 
kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama vivimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hive hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.
Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani  pekee huathiri watu zaidi ya milioni kumi na saba..Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe (adolescents) .Karibu asilimia 85 ya  vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na  zaidi ya  asilimia 20 ya wanawake  wenye umri wa zaidi ya miaka  ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe
.Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;
 • UMRI – Kama nilivyosema hormone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubalehe.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa  nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
 • VIPODOZI –Baadhi ya vipodozi kama Make-up za kina dada na Sprays za nywele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
 • CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufanya chunusi kuwa nyingi zaidi.
 • DAWA-Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na makusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
 • MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana.
 • MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye  mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
 • JINSIA-Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.
 • FAMILIA- Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia  wa familia kadhaa kuliko nyingine.
 • HOMONI- Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
 • USAFI WA MWILI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele  husababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwilini au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi
 • MAWAZO AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi vimkemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huweza kuchangia au kusababisha chunusi
 •  
  MATIBABU
  Matibabu ya chunusi yanajumuisha  kupunguza utoaji wA anta (sebamu ),kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingia au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyoeleza hapo juu.
  DAWA ZA KUPAKA
  Kuna dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi.Dawa hizi hupatikana kama cream,lotion,gel au pad.Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu. Mojawapo ya dawa hizi ni antibiotic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin na betamethasone au dexamethasone kama vile Gentrisone au Gentriderm cream,Erythromycin,B-Tex na kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa ukianza na asilimia ndogo (2.5%) na kuendelea kadri ngozi yako inavyohimili dawa. Gentamycin huua wadudu  wanaosababisha chunusi wakati dawa nyingine huondoa mwasho.
  Dawa nyingine ni zile zinzolainisha nta au Comedolytics na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi
  Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi  na sobuni ya kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.
  DAWAZA KUMEZA
  Wakati mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa kutumia dawa za kumeza kulingana na  wingi au ukubwa wa tatizo.Dawa kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi ,dawa hizo ni kama vile Erythromycin topical, Accutane (isotretinoin), Benzamycin Cleocin T (clindamycin phosphate), Desquam-E (benzoyl peroxide) Minocin (minocycline hydrochloride) na si vema kujinunulia mwenyewe tu na kuanza kutumia bila ushauri wa daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi.
  Wanawake wenye chunusi zisizotibika wanaweza kupewa Anti-androgens  kama vile baadhi ya vidonge wa uzazi wa mpango.Chunusi sugu hutibiwa kwa ciorticosteroids na anti-iflammatory drugs ambazo hutibu chunusi sugu ambazo huitwa Acne fulminans na hupatikana zaidi kwa vijana.
  MATIBABU MENGINE
  Kwa nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata  upasuaji mdogo (skin grafting) au plastic surgery kama chunusi imesababisha baka kubwa na kuna njia kama vile Chemical peel ambapo kemikali hupakwa kwenye ngozi na inapokauka kipande au gamba la juu la ngozi huondolewa na kuondoa baka.
  MATIBABU MBADALA
  Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.
  Watu wenye chunusi wanashauriwa  kulwa mlo kamili wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi,matunda , mboga za majani,vitamin B complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa,tumbaku,sukari,vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi
  HII YAFAA ZAIDI/  
  ONDOA CHUNUSI KWA DAWA YA ASILI,,,,


  Ukitaka kuondoa chunusi usoni na kusafisha uso usiwe na madoa kwa kiasili, njia zifuatazo zaweza sana kusaidia.Tafuta ukwaju loweka katika maji ukishalainika changanya na asali, paka usoni.
  Ni dawa nzuri sana na utaona ngozi yako inabadilika kwa kipindi kifupi.
  Kama utashindwa kupata vitu hivyo tafuta sabuni pamoja na krimu yenye mchanganyiko wa asali na ukwaju....lakini nadhani asali na ukwaju kama utaenda sokoni ni rahisi kupata,fanya hivyo ili upate amani ya moyo ndugu yangu.
 •  Ukitaka kuondoa chunusi usoni na kusafisha uso usiwe na madoa ni vyema ukatumia njia asili kufanya hivyo tumia asali na ukwaju kupata matokeo mazuri bila madhara 
 •  Ukwaju na asali hupatikana kwa urahisi sokoni
 •  Ipende ngozi yako wakati wote kama utaona inakuchukua muda mrefu kutengeneza mchanganyiko wa asali na ukwaju basi ni vyema vipodozi unavyonunua kama sabuni ama losheni hakikisha vimetengenezwa kwa mchanganyiko wa asali na ukwaju
 • Tafuta ukwaju loweka katika maji ukishalainika changanya na asali, paka usoni. muda mzuri wa kufanya hivi ni usiku  ambapo unapaka na kukaa takribani kama nusu saa kisha safisha uso wako vizuri fanya hivyo mara kwa mara kwani ni dawa nzuri sana na utaona ngozi yako inabadilika kwa kipindi kifupi.
 • NB; 
 • Chunusi haziwezi kutibika kabisa  japokuwa iwapo matibabu atakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona  na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.
  MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI
  Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
 • Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi  kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu.
 • Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na mafuta mgando
 •  Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
 • Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
 • Usibinye au kutoboa  vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
 • Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
 • Punguza mawazo

No comments: