Thursday, July 12, 2012

LOVE

 MAPENZI.
JIFUNZE KUTOA NA KUPOKEA RAHA ILI UFURAHIWE NA MWENZI WAKO…

Thamini Ubunifu Wa Mwenzako Kwa Kuonyesha Mapokeo

Watu Wanaingia Kwenye Uhusiano Kwa Sababu Ya Kusaka Watu Wa Kushirikiana Nao Katika Mambo Mbalimbali Yenye Kuleta Raha, Sio Vinginevyo. Unapokuwa Kwenye Uhusiano, Unapaswa Kufanya Kila Uwezalo Kuhakikisha Mwenzi Wako Anafurahishwa Na Yale Ambayo Unayafanya.

Ni Suala La Msingi Kwa Kila Mwenye Mpenzi, Kuwaza Namna Gani Afanye Ili Amfurahishe Mwenzi Wake. Ni Makosa Makubwa Kwa Mfano Mtu Kuamini Kwamba Njia Pekee Ya Kumfurahisha Mwenzi Wake Ni Kumpa Fedha, Kumnunulia Chakula Na Mambo Mengine Kama Haya, Bali Watu Walio Kwenye Mapenzi, Kitu Cha Kwanza Kabisa Cha Muhimu Kwao Ni Kuamini Kuwa Anaye Mtu Ambaye Anamjali, Anajali Hisia Zake Na Mambo Mengine Kama Haya Yanayohusiana Hasa Na Mapenzi.

Kuna Watu Wamekuwa Wakifikiri Kuhonga Magari Ndio Maana Ya Mapenzi, Lakini Sio Sahihi.Unaweza Kuhonga Na Bado Unachohonga Mwanaume Au Mwanamke Mwingine.
Hitaji La Kwanza Na La Msingi Sana Kwa Watu Walio Kwenye Mapenzi, Ni Kuushika Moyo Wake, Uamini Kuwa Unampenda Na Unahangaika Kusaka Njia Za Kumridhisha Kwa Mambo Mbalimbali. Mapenzi Yanajengwa Na Kauli; Ni Jambo La Msingi Sana Kwa Wanandoa Au Watu Walio Kwenye Uhusiano Kutoleana Kauli Nzuri.

Kauli Za Kuheshimiana, Badala Ya Kutukanana Au Kutoleana Dharau Za Aina Mbalimbali. Je, Wewe Kauli Unazomtolea Mwenzi Wako Ungezifurahia Kutolewa? Kutoa Kauli Za Matusi, Dharau Na Mambo Mengine Kama Haya Ni Vitu Vinavyokatisha Tamaa.

Wakati Mwingine Unaweza Kuringa Kwamba Acha Nimfanyie Fulani Mambo Kadri Ninavyotaka Yawezekana Ni Kumuendesha Kama Gari Bovu, Lakini Mapenzi Si Fedha, Mapenzi Ni Ile Hali Ya Kumfanya Mtu Kupata Amani. Mapenzi Yanamuhitaji Mtu Kuzingatia Matendo Mazuri Ya Kutiana Moyo.

Kwa Bahati Mbaya Wapo Watu Wanapigana Hadharani, Kwao Wanaona Ni Sawa. Kuna Watu Wamekuwa Wakifanyiana Mambo Mbalimbali Ambayo Hata Ukimuuliza Mfanyaji. Je, Vipi Unafurahi Kama Ungefanyiwa, Jibu Ni Kwamba Hayuko Tayari Kufanyiwa. Kimsingi Watu Walio Kwenye Uhusiano Wanapaswa Kufanyiana Mambo Mazuri. Kwa Mfano Wanaume Wengi Wamekuwa Na Umimi Katika Suala Zima La Mahaba; Kwamba Hawana Wa Kufurahiana Na Wenzi Wao Au Kuwapa Nafasi Kufanya Wanavyotaka.

Baadhi Wakifanya Vitu Vipya Wanaambiwa, Aaah Tayari Umeshaanza Kuwa Malaya, Haya Mambo Umeyatoa Wapi? Lakini Akifanya Mwanaume Aaaah Hakuna Tatizo. Ndio Nasema Ni Suala La Msingi Watu Walio Kwenye Mapenzi, Kufanyiana Mambo Mazuri.
Mahaba Ni Jambo Ambalo Linapaswa Kufanywa Kwa Ustadi Mkubwa, Kwa Kujaliana, Lakini Zaidi Ya Yote Ni Lazima Wahusika Wote Wawe Katika Hali Ya Kufanya, Sio Kulazimishana Kama Ambavyo Baadhi Ya Watu Wamekuwa Wakifanya. Kuna Wengine Hata Kama Hakuna Maandalizi, Anakuvamia, Ukisema Mbona Inakuwa Hivi Kama Una Haraka Unaweza Kwenda Halafu Tukaonana Baadaye, Si Wengi Ambao Wanaweza Wakakuelewa.

Msingi Wa Kufurahia Ndoa Ni Pamoja Na Wanandoa Wenyewe Kujijua Kwamba Nikoje Na Mwenzi Wako Anataka Nini Au Nini Cha Kufanya Ili Aweze Kufurahia. Unatakiwa Kuujua Mwili Wako, Na Kujua Namna Ya Kufanya. Hakuna Haja Ya Kufichana Chochote.Kwa Vyovyote Itakavyokuwa Raha Ya Mapenzi, Huwa Inachangiwa Na Namna Ambavyo Mtu Unayeshiriki Naye Unampenda Au La.

Ni Muhimu Kumpa Nafasi Mwenzi Wako Afurahie Ndoa Yenu, Wala Hakuna Sababu Ya Kutesana Au Kunyimana Raha Kwa Vitu Ambavyo Vinapatikana. Kama Unafikiri Watu Wanaoana Ili Kutafuta Magari, Kupewa Fedha Au Mambo Mengine Kama Haya, Ni Dalili Kwamba Kichwa Chako Kinahitaji Mafunzo Zaidi.

MAPENZI HAYAPATIKANI KWA KUHONGA..

No comments: