LOVE
MAPENZI.
JIFUNZE KUTOA NA KUPOKEA RAHA ILI UFURAHIWE NA MWENZI WAKO…
Thamini Ubunifu Wa Mwenzako Kwa Kuonyesha Mapokeo
Watu Wanaingia Kwenye Uhusiano Kwa Sababu Ya Kusaka Watu Wa
Kushirikiana Nao Katika Mambo Mbalimbali Yenye Kuleta Raha, Sio
Vinginevyo. Unapokuwa Kwenye Uhusiano, Unapaswa Kufanya Kila Uwezalo
Kuhakikisha Mwenzi Wako Anafurahishwa Na Yale Ambayo Unayafanya.
Ni Suala La Msingi Kwa Kila Mwenye Mpenzi, Kuwaza Namna Gani Afanye Ili
Amfurahishe Mwenzi Wake. Ni Makosa Makubwa Kwa Mfano Mtu Kuamini Kwamba
Njia Pekee Ya Kumfurahisha Mwenzi Wake Ni Kumpa Fedha, Kumnunulia
Chakula Na Mambo Mengine Kama Haya, Bali Watu Walio Kwenye Mapenzi, Kitu
Cha Kwanza Kabisa Cha Muhimu Kwao Ni Kuamini Kuwa Anaye Mtu Ambaye
Anamjali, Anajali Hisia Zake Na Mambo Mengine Kama Haya Yanayohusiana
Hasa Na Mapenzi.
Kuna Watu Wamekuwa Wakifikiri Kuhonga Magari
Ndio Maana Ya Mapenzi, Lakini Sio Sahihi.Unaweza Kuhonga Na Bado
Unachohonga Mwanaume Au Mwanamke Mwingine.
Hitaji La Kwanza Na La
Msingi Sana Kwa Watu Walio Kwenye Mapenzi, Ni Kuushika Moyo Wake, Uamini
Kuwa Unampenda Na Unahangaika Kusaka Njia Za Kumridhisha Kwa Mambo
Mbalimbali. Mapenzi Yanajengwa Na Kauli; Ni Jambo La Msingi Sana Kwa
Wanandoa Au Watu Walio Kwenye Uhusiano Kutoleana Kauli Nzuri.
Kauli Za Kuheshimiana, Badala Ya Kutukanana Au Kutoleana Dharau Za Aina
Mbalimbali. Je, Wewe Kauli Unazomtolea Mwenzi Wako Ungezifurahia
Kutolewa? Kutoa Kauli Za Matusi, Dharau Na Mambo Mengine Kama Haya Ni
Vitu Vinavyokatisha Tamaa.
Wakati Mwingine Unaweza Kuringa
Kwamba Acha Nimfanyie Fulani Mambo Kadri Ninavyotaka Yawezekana Ni
Kumuendesha Kama Gari Bovu, Lakini Mapenzi Si Fedha, Mapenzi Ni Ile Hali
Ya Kumfanya Mtu Kupata Amani. Mapenzi Yanamuhitaji Mtu Kuzingatia
Matendo Mazuri Ya Kutiana Moyo.
Kwa Bahati Mbaya Wapo Watu
Wanapigana Hadharani, Kwao Wanaona Ni Sawa. Kuna Watu Wamekuwa
Wakifanyiana Mambo Mbalimbali Ambayo Hata Ukimuuliza Mfanyaji. Je, Vipi
Unafurahi Kama Ungefanyiwa, Jibu Ni Kwamba Hayuko Tayari Kufanyiwa.
Kimsingi Watu Walio Kwenye Uhusiano Wanapaswa Kufanyiana Mambo Mazuri.
Kwa Mfano Wanaume Wengi Wamekuwa Na Umimi Katika Suala Zima La Mahaba;
Kwamba Hawana Wa Kufurahiana Na Wenzi Wao Au Kuwapa Nafasi Kufanya
Wanavyotaka.
Baadhi Wakifanya Vitu Vipya Wanaambiwa, Aaah
Tayari Umeshaanza Kuwa Malaya, Haya Mambo Umeyatoa Wapi? Lakini Akifanya
Mwanaume Aaaah Hakuna Tatizo. Ndio Nasema Ni Suala La Msingi Watu Walio
Kwenye Mapenzi, Kufanyiana Mambo Mazuri.
Mahaba Ni Jambo Ambalo
Linapaswa Kufanywa Kwa Ustadi Mkubwa, Kwa Kujaliana, Lakini Zaidi Ya
Yote Ni Lazima Wahusika Wote Wawe Katika Hali Ya Kufanya, Sio
Kulazimishana Kama Ambavyo Baadhi Ya Watu Wamekuwa Wakifanya. Kuna
Wengine Hata Kama Hakuna Maandalizi, Anakuvamia, Ukisema Mbona Inakuwa
Hivi Kama Una Haraka Unaweza Kwenda Halafu Tukaonana Baadaye, Si Wengi
Ambao Wanaweza Wakakuelewa.
Msingi Wa Kufurahia Ndoa Ni Pamoja
Na Wanandoa Wenyewe Kujijua Kwamba Nikoje Na Mwenzi Wako Anataka Nini Au
Nini Cha Kufanya Ili Aweze Kufurahia. Unatakiwa Kuujua Mwili Wako, Na
Kujua Namna Ya Kufanya. Hakuna Haja Ya Kufichana Chochote.Kwa Vyovyote
Itakavyokuwa Raha Ya Mapenzi, Huwa Inachangiwa Na Namna Ambavyo Mtu
Unayeshiriki Naye Unampenda Au La.
Ni Muhimu Kumpa Nafasi
Mwenzi Wako Afurahie Ndoa Yenu, Wala Hakuna Sababu Ya Kutesana Au
Kunyimana Raha Kwa Vitu Ambavyo Vinapatikana. Kama Unafikiri Watu
Wanaoana Ili Kutafuta Magari, Kupewa Fedha Au Mambo Mengine Kama Haya,
Ni Dalili Kwamba Kichwa Chako Kinahitaji Mafunzo Zaidi.
MAPENZI HAYAPATIKANI KWA KUHONGA..
No comments:
Post a Comment