KUNYONYESHA HUPUNGUZA UWEZEKANO MKUBWA KUPATA KANSA YA MATITI;
Mbali na ukweli kwamba kunyonyesha ndiyo chanzo cha lishe bora kabisa
kwa mtoto, wanasayansi sasa wanadai kwamba kunyonyesha pia kunaweza
kupunguza uwezekano wa mama kupata kansa ya matiti kwa asilimia 25 hadi
60.
Hizi ni habari njema kwa akina mama wa Afrika ambao kimsingi
huchukulia kunyonyesha kama mojawapo ya wajibu wao baada ya kupata
mtoto. Pengine hii inaweza kuwa ndiyo sababu iliyofanya saratani ya
matiti isijidhihirishe sana Afrika.
Wasiwasi wangu ni juu ya
kizazi kipya ambacho kinaiga mambo ya Kimagharibi kwa pupa. Nimeshasikia
kwamba mabinti wengi sasa hawana hamu tena ya kunyonyesha vichanga vyao
wakichelea kuharibu matiti na miili yao. Ukijumlisha na vitu vingine
vinavyoingia Afrika vikiwemo vyakula vilivyolimwa "kisayansi", madawa na
mabadiliko mazima ya mfumo wetu wa maisha, sitashangaa kama kansa
itafumuka na kuwa ugonjwa wa kawaida tu muda si mrefu ujao. Hili
likitokea, atakayefaidika bila shaka ni makampuni ya madawa ya nchi za
Kimagharibi - na naamini kwamba hiki ndicho wanachotaka. Tuweni
waangalifu na tuache mambo ya kuiga vitu kiholela bila kuelewa hasa
kiini chake.
No comments:
Post a Comment