Thursday, October 17, 2013

BAADA YA CHAKULA EPUKA HAYA.


HUTAKIWA KUFANYA MAMBO HAYA BAADA YA KULA CHAKULA.


1;USIVUTE SIGARA
Ni dhahiri kuwa sigara ina madhara kiafya, kwa ujumla wake watu wanashauriwa kuacha kutumia. 
Lakini inaelezwa kuwa madhara yake huongezeka mara kumi iwapo mvutaji atavuta mara baada ya kula chakula. 

Utafiti wa kimaabara unaonesha kuwa ukivuta sigara moja baada ya kula ni sawa na mtu aliyevuta sigara 10, hivyo hatari ya kupata saratani huongezeka.
2; USILE MATUNDA
. Usile matunda baada ya mlo kwani ulaji huo hulifanya tumbo kujaa hewa na matokeo yake kusababisha gesi tumboni. 


Usahihi ni kula matunda saa moja au mbili kabla au baada ya kula chakula chako.  Kula matunda muda mfupi tu mara baada ya kula chakula ni kosa ambalo linafanywa na watu wengi na huonekana ni sawa.
3;USINYWE CHAI.
Mara baada ya kula chakula, iwe mchana au usiku, usinywe chai. Kwa mujibu wa utafiti, majani ya chai yana kiwango kikubwa cha tindikali (acid), hivyo unapokunywa chai tindikali hiyo hufanya protini iliyo kwenye chakula ulichokula kuwa ngumu na hivyo kutosagika tumboni haraka, matokeo yake ni mtu kukosa choo kwa siku kadhaa.

4;
USILEGEZE MKANDA
Unaweza usilichukulie ‘serious’ jambo hili, lakini ni jambo la hatari kwa mustakabali wa afya ya mtu. Mara baada ya kula, usilegeze mkanda wa suruali yako, uache kama ulivyokuwa hapo awali kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha utumbo kujikunja na kuziba.
5; USIOGE.

Usioge baada ya kula, bali oga kabla ya kula. Inaelezwa kuwa unapooga baada ya kula, mtiririko wa damu huongezeka zaidi sehemu za mikono, miguu na mwili na kusababisha damu kupungua sehemu za tumboni. 


Damu inapopungua tumboni maana yake ni kudhoofika kwa mfumo wa usagaji chakula tumboni (digestive system).
6; USILALE
Usilale muda mfupi tu mara baada ya kula, kwani chakula ulichokula hakitaweza kusagwa sawaswa na huweza kusababisha vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya kuambukiza kwenye utumbo mdogo.

No comments: